Mbaroni kwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha 3 Pwaga
20 July 2026, 17:47

Hadi sasa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea chini ya uongozi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mpwapwa.
Na Stephen Noel.
Watu watatu wakazi wa Kijiji cha Pwaga, Kata ya Pwaga Wilaya ya Mpwapwa wanashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani humo kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Pwaga.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji wa Kata ya Pwaga, Bi. Moteswa Mnyabwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari mtuhumiwa mmoja amekamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Mpwapwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Pwaga, Jastini Maganga amesema shule imetoa msaada wa ushauri wa kisaikolojia kwa mwanafunzi huyo ili kusaidia kurejesha hali yake.
Maganga amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao na kufuatilia mienendo yao kila siku.