Dodoma FM

Wakulima Kongogo waahidiwa mashine za kisasa

27 April 2023, 6:54 pm

Mashine ya kisasa ya kupandia Mpunga. Picha na Mindi Joseph.

Na Mindi Joseph.

Mbunge wa Jimbo la Bahi, Kenneth Nollo amewaahidi wakulima wa Kongogo kuwanunulia mashine za kisasa za kupandia mpunga pindi tu ujenzi wa skimu ya umwagiliaji utakapokamilika 2024.

Akizungumza na Wakulima hao amesema wilaya ya bahi imekuwa ikizalisha mpunga kwa wingi hivyo mashine hizo zitawasaidia wakati wa kupanda.

Mh Nollo amesema Mashine hizo zitawarahisishia wakulima kupanda kwa kisasa kuondokana na mfumo wanaoutumia wa zamani.

Sauti ya mh. Nollo

Mashine hizo njia bora kwa wakulima wa mpunga kwani wengi wa wakulima bado wanatumia zana duni za kilimo.