Dodoma FM

Serikali yazindua kituo cha umahiri wa masuala ya afya kidigitali

15 August 2023, 2:32 pm

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amezindua Kituo cha Umahiri katika masuala ya afya kidigitali (Center for Digital Health).Picha na Alfred Bulahya.

Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Afya Bw. Silvanus Ilomo amefafanua namna kituo hicho kitakavyosaidia kuboresha huduma za afya.

Na Alfred Bulahya.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amezindua Kituo cha Umahiri katika masuala ya afya kidigitali (Center for Digital Health) kitakachosaidia kuchagiza ubunifu wa TEHAMA kwenye Sekta ya Afya.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma ambapo katika hafla hiyo Dkt Shekalaghe ametoa maagizo kwa watumishi kuhakikisha kituo hicho kinatumika kuunganisha mifumo kidigital kwa hospitali zote ili kusadia utoaji wa huduma kwa jamii.

Sauti ya Dkt. Seif Shekalaghe .

Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Afya Bw. Silvanus Ilomo amefafanua namna kituo hicho kitakavyosaidia kuboresha huduma za afya na sekta nyingine nchini.

Sauti ya Bw. Silvanus Ilomo.
Picha Dkt. Seif Shekalaghe akizindua kituo hicho. Picha na Alfred Bulahya.

Amos Mugisha ni Mkurugenzi mkazi kutoka shirika la PATH, ambalo limekuwa likifanya kazi za utekelezaji wa Miradi mbalimbali nchini amesema kituo hicho kimejengwa kwa kuwezesha na shirika hilo huku akieleza umhimu wa kituo hicho.

Sauti ya Amos Mugisha.