Dodoma FM

Wajawazito wahimizwa kutumia dawa kinga

6 September 2023, 1:47 pm

Ni muhimu kwa akina mama kupata dawa kinga hususani dawa kinga ya malaria pamoja na minyoo. Picha na google.

Kwa mujibu wa wataalam wa afya, wanasisitiza suala la akina mama kupata dawa kinga kwani zimekuwa na umuhimu kwa afya ya mama na mtoto.

Na Naima Chokela.                    

Imeelezwa kuwa upo umuhimu kwa mama mjamzito kupatiwa dawa kinga katika kipindi cha ujauzito ambapo itamsaidia katika suala la ukuaji bora wa afya ya mtoto na mama kujifungua salama.

Hayo yamesemwa na muuguzi kutoka katika hospitali ya Makole Bw. Nchimbi Januari wakati akitoa elimu kwa akina mama waliohudhuria kliniki kupata huduma mbalimbali za kiafya.

Amesema kuwa ni muhimu kwa akina mama kupata dawa kinga hususani dawa kinga ya malaria pamoja na minyoo ambapo itamsaidia katika kumlinda mama pamoja na mtoto.

Sauti ya Nchimbi Januari Afisa Muuguzi
Picha ni aina mbalimbali za dawa kinga anazotakiwa kutumia mama mjamzito. Picha na UN News.

Aidha amewataka akina mama kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kupata elimu juu ya suala hilo kwa kuhudhuria kliniki ili kuepukana na magonjwa yanayoweza kujitokeza baadaye.

Sauti ya Nchimbi Januari Afisa Muuguzi

Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya wananchi juu ya umuhimu wa suala la kuwahi kliniki kwa ajili ya kupata elimu juu ya suala hili pamoja na elimu juu ya masuala mengine nao wakawa na haya ya kusema.