Dodoma FM

Buriani Magufuli Dodoma haitakuona tena

23 March 2021, 6:23 am

Na; Mariam Kasawa.

Hatimaye zoezi la kuuaga mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli limekamilika Jijini Dodoma na sasa ni zamu ya Zanzibar.

Leo Machi 23 2021 wananchi wa Zanzibar watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa rais hayati Dkt. John Magufuli .

Baada ya zoezi hilo kukamika Zanzibar litahamia jijini Mwanza ambapo wananchi watatoa heshima za mwisho Machi 24 na baadae kuelekea Chato  Mkoani Geita kwaajili ya wanafamili na wananchi kutoa heshima zao za mwisho na mazishi ambayo yanatarajia kufanyika Machi 26.

Endelea kutembelea ukurasa wetu kwa habari zaidi kuhusu tukio hili.