Dodoma FM

Wakazi wa Magaga waiomba serikali kuwatatulia changamoto ya barabara

27 May 2022, 3:22 pm

Na;Mindi Joseph.

Wananchi wa kitongoji cha Magaga wameiomba serikali kuwatatulia changamoto ya miundombinu ya Barabara Kutoka Magaga kuelekea Mvumi pamoja na kuwajengea Daraja.

Wakizungumza na taswira ya habari wamesema changamoto hii inawaathiri katika shughuli zao za maendeleo na wameomba Serikali kuwatengenezewa barabara hiyo.

Wameongeza kuwa mbali na hiyo barabara wanakabiliwa na changamoto ya daraja ambalo licha ya kufanyiwa ukarabati linabomoka mara kwa mara

.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  kitogoji cha magaga Bw Samweli Palwase amesema jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika kuhakikisha Daraja hilo linafanyiwa ukarabati.

.

Daraja hilo lililopo kitongoji cha Magaga limekuwa likifanyiwa ukarabati lakini wakati wa masika linabomoka na miumndombinu yake kuharibiwa na mvua.