Dodoma FM

Vijana wakumbushwa kujiwekea akiba

10 April 2023, 3:19 pm

Mmoja wa vijana hao akizungumza na Dodoma Tv. Picha na Thadey Tesha.

Mara kadhaa kumekuwepo na baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakihinda vijiweni pasipo kuwa na ajira huku wengi wao wakisema kuwa mitaji ni miongoni mwa changamoto zinazopelekea kushindwa kujiajiri.

Na Thadei Tesha.

Vijana wametakiwa kutumia vyema nafasi waliyonayo katika kuwekeza kidogo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi ilikuondokona na changamoto ya ukosefu wa ajira.

Hayo yamesemwa na baadhi ya vijana ambao ni wajasiriamali pamoja na wabunifu katika mahojiano maalum wakati walipotembelea kituo cha Dodoma tv.

wamesema ili vijana waweze kunufaika kiuchumi ni vyema wao wenyewe kujitambua  kwa kuweka akiba pamoja na kuonyesha bidii na uthubutu wa  kile walichonacho na katika kutumia fursa zinazowazunguka huku jamii ikitakiwa kutoa sapoti.

Sauti za vijana

Aidha mmoja wa wajasiriamali hao Bi elizabeth obeid yeye ni mjasiramali wa kutengeneza mavazi pamoaja na pochi kwa kutumia uzi wa kufuma kwa mkonio hapa anatuelezea uzoefu wake katika sjhughuli hiyo.

Sauti ya Mjasiriamali