Dodoma FM

Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) lazindua kanzi data ya wafanyabiashara wa Tanzania

20 September 2021, 11:42 am

Na; Mariam Matundu .

Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC)linatarajia kuzindua Kanzi data ya wafanyabiashara wa Tanzania ili kuongeza wigo wa uwekezaji.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo Beng’i Issa wakati alikitoa taarifa juu ya Kongamano la 5 la mwaka la uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Amesema kupitia kanzi data hiyo itasaidia wafanyabiashara na makampuni ya ndani kujulikana kimataifa hali itakayosaidia kukuza uwekezaji.

Aidha amesema kupitia kongamano hilo watapata nafasi ya kupima utekelezaji wa sera ya uwekezaji wananchi kiuchumi pamoja na shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Nae mwenyekiti wa kongamano hilo Suleiman Malela amesema kuwa kongamano hilo ni muhimu kwa kuwa litawaweza kuwakutanisha wadau mbalimbali na kufungua fursa zitakazoleta maendeleo.

Kongamano la 5 la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi linatarajiwa kifanyika Jijini Dodoma October 4 mwaka huu ambapo mgeni rasmi atakuwa ni waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassimu Majaliwa .