Dodoma FM

Ratiba ya kuaga Mwili wa Rais Magufuli Dodoma yabadilishwa

22 March 2021, 7:55 am

Na; Mariam  Kasawa.

Baada ya uongozi wa mkoa wa Dodoma kutambua hamu ya wakazi wa  jiji hili ya kutamani kumuaga Hayati Dkt John Pombe Magufuli  wameamua kuzunguka maeneo mbalimbali ili kila mwananchi aweze kushiriki zoezi hili.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Jamuhuri  mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilithi Mahenge amesema kama Mkoa wameona ni vema kutoa fursa kwa kila mwananchi kushiriki zoezi la kuaga  hivyo wametengeneza mitaa ambayo magari ya msafara wa mwili huo yata pita.

Amesema baada ya makundi maalum kupata nafasi ya kuaga katika uwanja wa Jamuhuri magari hayo yatazunguka sehemu zifuatazo.

 Raund abaut ya Bahi, barabara ya kuelekea Iringa wakipitia Mirembe, barabara ya kito baa hadi centrol Polisi, barabara ya Jamatini, Morena, Emmaus,  Barabara ya kwa waziri Mkuu, African Dream,  na wajenzi baada ya hapo msafara utarudi uwanja wa ndege wa Dodoma.