Dodoma FM

Hali mbaya ya hewa yachangia ongezeko la majanga ya asili

13 October 2021, 2:02 pm

Na; Fred Cheti.

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia majanga ya asili duniani ripoti kutoka umoja wa mataifa inataja kuwa hali mbaya ya hewa ni chanzo kinachosababisha ongezeko la majanga hayo ya asili katika karne hii ya 21.

Ripoti hiyo iliyotolewa Oktoba mwaka jana na ofisi ya umoja wa mataifa ya kupunguza madhara ya majanga, UNDRR inasema kati ya mwaka 2000 na 2019 kulikuwepo na matukio 7348 ya majanga yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya milioni 1.2 huku wengine bilioni 4.2 maisha yao yakiathiriwa na majanga hayo.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi jijini hapa ili kufahamu ni kwa namna gani wanaondoka na uchafuzi wa hewa pamoja na mazingira na hewa ambayo ndio chanzo kikubwa cha kutokea kwa majanga hayo katika karne hii ya 21.

Kwa upande wake afisa mazingira na udhibiti wa taka ngumu kutoka jiji la Dodoma Bw. Dickson Kimaro amewataka wananchi wa jiji la Dodoma kuacha tabia ya uchomaji miti na misitu hovyo ili kuepuka uchafuzi wa hewa badala yake wawe na utaratibu wa kupanda miti katika maeneo yao ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Majanga ya asili ni matukio ambayo hutokea bila kuingilia kati kwa binadamu ambayo huleta maafa makubwa kwa maisha ya binadamu ambayo husababishwa na hali ya hewa, michakato ya geomofolojia, sababu za kibaolojia au hali ya anga.Mara nyingi, wanadamu wanawajibika kwa athari za maovu ya kiufundi, uzembe, au matokeo ya mipango mibaya.