Dodoma FM

Tunashindwa kuelewa juu ya mfumo wa Bima ulivyo

3 February 2023, 4:36 pm

Bima ya CHF iliyoboreshwa.Picha na chf-imis

Imeelezwa kuwa licha ya mikakati mbalimbali ya uboreshwaji wa huduma za afya bado wananchi wameendelea kulalamika huduma ya bima ya CHF iliyoboreshwa.

Na Victor Chigwada

Wananchi wa Kata ya Mlowa Barabarani wamesema kuwa wanashindwa kuelewa mfumo wa bima ulivyo ,kutokana na walio wengi wanapoenda kupata matibabu katika vituo vya afya au zahanati kulazimika kwenda kununua dawa.

Wananchi wa Kata ya Mlowa .

Nae Mwenyekiti wa kijiji cha Mloda Bw.Adamu Philimini amesema kuwa

“licha ya hamasa ya bima lakini kumekuwa na malalamiko kadhaa juu ya matibabu kupitia mfumo wa bima”

Mwenyekiti Bw.Adamu Philimini.

Aidha Diwani wa Kata hiyo Bw.Anjero Lukasi amekiri kuwa hamasa ya ukataji bima imeendelea kupungua kwa wananchi wa Kata ya Mlowa Barabarani

“kutokana na changamoto ya kukosekana kwa dawa kwa baadhi ya zahanati na vituo vya afya”

Diwani Bw.Anjero Lukasi.