Dodoma FM

Tatizo la afya ya ngozi latajwa kuchangia muwasho wa jicho

21 December 2023, 5:47 pm

Picha ni Katibu mkuu wa Taasisi ya Tiba ya macho ijulikanayo kama Tanzania Optrometric Association dk Salum salum.Picha na Aisha Alim.

Dkt. Salumu amesema matatizo ya ngozi pamoja na matumizi ya sabuni za aina tofauti husababisha mtu kupatwa na tatizo hilo.

Na Aisha Alim.

Tatizo la macho kupatwa na muwasho linataja kusababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo tatizo la afya ya ngozi

Katibu mkuu wa taasisi ya Tiba ya macho ijulikanayo kama Tanzania Optrometric Association Dkt. Salum Salum amebainisha hayo wakati akizungumza na kituo hiki juu ya tatizo la macho kuwasha.

Sauti ya Dkt. Salum Salum.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na kituo hiki juu ya uelewa wa tatizo hilo wametaja njia ambazo huzitumia kujikinga na tatizo hilo ikiwemo kuepuka kukaa eneo linapovuka moshi.

Sauti za baadhi ya wananchi.

Dokta salumu salumu amewashauri wananchi kuwahi mapema kwa wataalamu wa magonjw ya macho pindi wanapobaini dalili za macho kuwasha ili wapatiwe msaada mapema.

Sauti ya Dkt. Salum Salum.