Dodoma FM

Ujenzi wa bweni Chamwino waanzishwa kuwalinda wasichana na mimba

5 May 2025, 18:23

Picha ni wazazi wakiwa katika mkutano shuleni hapo. Picha na Wilaya ya Chamwino.

Hayo yamebainishwa katika kikao Cha kujadili Maendeleo ya Shule ya Sekondari Chinangali kilicho fanyika may 3.

Na Annuary Shaban.
Kata ya Chamwino-Halmashauri ya jiji la Dodoma, imeanza mchakato wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike kwa nguvu za wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Hayo yamebainishwa katika kikao Cha kujadili Maendeleo ya Shule ya Sekondari Chinangali kilicho fanyika may 3.

Sambamba na Mambo mengine kujadiliwa, kikao hicho kilijikita kujadili Maendeleo ya Shule hasa namna ya kuanzisha ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wa Kike ambapo umelenga kumlinda Mtoto wa Kike dhidi ya Mimba za utotoni na zisizotarajiwa pamoja na kupunguza utoro shuleni hapo.

Picha ni wazazi wakiwa katika mkutano shuleni hapo. Picha na Wilaya ya Chamwino.

Mgeni Rasmi wa Kikao hicho alikua ni Diwani wa Kata ya Chamwino Mhe.Jumanne Ngede ambaye aliambatana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino Ndugu Lucas Venance.

Aidha, Uamuzi kuleta wazo la kuanzisha ujenzi bweni hilo umefikiwa katika kikao cha pamoja Cha wataalamu wa Ngazi ya Kata na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chamwino wakati wa kuwasilisha,kupitia na kujadili Taarifa ya miaka Minne ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Serikali ya Kata.

Mwisho, Wazazi/Walezi wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari Chinangali wamekubali kuchangia mchango ili kujenga Bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike ili kusaidia kufikia Malengo na ndoto zao.