Dodoma FM

Vijana nchini wametakiwa kufuatilia matangazo ya kujiunga na vyuo mbalimbali ili kuongeza ujuzi

7 September 2021, 2:19 pm

Na; Selemani Kodima .

Vijana nchini wametakiwa kufuatialia kwa makini matangazo yanayotolewa na ofisi ya Waziri mkuu hususani ya kujiunga na vyuo mbalimbali ilikuongeza ujuzi.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa vijana bungeni pamoja na mwakilishi wa watu wenye mahitaji maalumu (walemavu) Bi Khadija Shaban baada ya kutembelea chuo cha marekebisho kwa watu wenye Ulemavu mkoani Singida.

Wakizungumza kwa Nyakati tofauti Wajumbe wa kamati hiyo ya kudumu ya Bunge la katiba na sheria wamewashauri Vijana kuwa wabunifu na kujitolea kujifunza ili kuwa na uwanda mpana wa kujiajiri kuliko kusubiri nafasi chache zinazotangazwa za ajira.

Kwa upande mwingine wamewataka jamii kuwashika mkono Vijana wote ambao wanatoka katika mafunzo ya ujuzi na fani kuwapa nafasi ili waweze kujiunua zaidi .

Pamoja na hayo Vijana na watu wenye Ulemavu wametakiwa kutotumia Ulemavu kama sehemu ya faida bali wanatakiwa kutumia fursa za nguvu na akili zao kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.