Dodoma FM

Wakazi wa Ntyuka wametakiwa kuacha kupitisha mifugo barabarani

16 December 2021, 1:57 pm

Na; Benard Filbert.

Wafugaji katika Kata ya Ntyuka jijini Dodoma wametakiwa kuacha kupitisha mifugo yao barabarani ili kuepuka uharibifu wa barabara.

Hayo yameelezwa na Diwani wa Kata hiyo Bw.Yona Mrema wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu utunzaji wa miundombinu ya barabara katika Kata ya Ntyuka.

Amesema baadhi ya barabara katika Kata hiyo zimekarabatiwa katika kiwango cha changarawe hivyo wafugaji wanatakiwa kupitisha mifugo pembezoni mwa barabara ili kuepuka ukarabati wa mara kwa mara.

Ameongeza kuwa ulinzi wa barabara unatakiwa kusimamiwa na kila mtu hivyo wanatakiwa kuwa walinzi na kufuata maagizo ya viongozi.

Serikali inajitahidi kukarabati miundombinu ya barabara katika maeneo mengi nchini ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi ambapo wananchi wanatakiwa kuzitunza.