Dodoma FM

NEC kuanza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura

13 November 2023, 2:47 pm

Picha ni baadhi ya vifaa vya zoezi hilo la uboreshaji wa daftari hilo. Picha na Mariam Kasawa.

Na Aisha Alim. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC inatarajia kuanza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa uchaguzi.  

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC Bw. Ramadhani Kailima wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kuwa zoezi hilo linatarajia kuanza tarehe 24 hadi tarehe 23 Novemba mwaka huu.

Sauti ya Bwana Ramadhani Kailima.
Picha ni Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi Bwana Ramadhani Kailima. Picha na Mariam kasawa.

Zoezi hili linafanyika kwa lengo la kupima uwezo wa vifaa na mifumo ya uandikishaji itakayotumika wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura unaotarajiwa kufanyika nchi nzima kwa tarehe na ratiba itakayopangwa na tume

Sauti ya Bwana Ramadhani Kailima.