Dodoma FM

Viongozi watakiwa kuacha kutumia nguvu za giza

9 October 2023, 8:36 pm

Picha ni mgeni rasmi akizindua kanisani hapo. Picha na Seleman Kodima.

Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Pentecoste Christian International Thomas Kiula wakati wa tukio la Uzinduzi wa kanisa jipya na kumsimika Uchungaji wa kanisa hilo linalopatikana mtaa Ndachi kata ya Mnadani Dodoma Mjini.

Na Seleman Kodima.

Viongozi wametakiwa kuacha kutumia Nguvu za Giza  wakati wakisaka nafasi ya Uongozi kupitia Chaguzi mbalimbali hapa nchini .

Akizungumza baada ya tukio hilo Askofu Kiula amesema wakati  Taifa tunaelekea uchaguzi wa mwaka 2024 ipo haja Viongozi wanaotumia Nguvu za giza kuanza kubadilika na kumtegemea Mungu ili kuwa na Utawala Bora wenye hofu na Mungu.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika Tukio hilo Diwani wa Kata ya Mnadani Paul Richard ambaye aliwakilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Aman Bw Mussa Daudi amesema viongozi wa Dini wana nafasi kubwa  ya kuombea Taifa na Viongozi.

Aidha amewataka Vijana kufanya kazi kwa bidii ili waweze kumtolea Mungu sadaka.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Mnadani Paul Richard
Picha ni Askofu wa kanisa hilo akiwasimika watumishi hao. Picha na Seleman Kodima.

Nae Mchungaji wa kanisa hilo ambaye amesimikwa Henry Masunyilo amewashukuru waumini wa kanisa hilo pamoja na wananchi wa eneo hilo kwa upekee na ushirikiano walionesha katika tukio hilo  adhimu.

Sauti ya Mchungaji wa kanisa hilo ambaye amesimikwa Henry Masunyilo

Katika Uzinduzi huo ,Askofu wa Kanisa hilo amefanya harambee ya Viti ambapo Jumla ya Viti 47 viliweza kutolewa na baadhi ya Viongozi wa Kidini pamoja na serikali ambapo Diwani wa kata ya Mnadani ameahidi kutoa shilingi laki Tano .

Sauti ya Askofu wa Kanisa hilo .