Dodoma FM

Yafahamu madhara ya kuweka simu karibu na kichwa wakati wa kulala

21 August 2023, 5:09 pm

Wataalamu wanashauri kuweka simu mbali mtu anapo lala ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea. Picha na Microsoft Bing.

Kwa mujibu wa chapisho la Ukurasa wa gazeti la Mwananchi la Febrauari 19,2021 linasema kuwa, Madaktari bingwa wa Ubongo na Mishipa ya fahamu na wale wa Magonjwa ya Saratani wanaonya kuwa kulala karibu na simu kuna madhara kiafya na kunaweza kusababisha mtu kupata Saratani .

Na Abraham Mtagwa.

Wanajamii wameshauriwa kuwa makini na matumizi ya simu hasa wakati wa kulala kwani kutofanya hivyo kunaweza kusababisha madhara kiafya.

Hayo yamesemwa na Bw. Stephano Daburu ambaye ni Mteknolojia na Mtaalamu wa Afya kutoka Jijini Dodoma na hapa anabainisha baadhi ya madhara ya kuweka simu maeneo ya kichwani hasa wakati wa kulala.

Sauti ya Stephano Daburu Mteknolojia
Wataalamu wanaonya kuwa kulala karibu na simu kuna madhara kiafya na kunaweza kusababisha mtu kupata Saratan ya ubongo. Picha na Microsoft Bing.

Aidha baadhi ya Watumiaji wa simu Jijini Dodoma wamekuwa na maoni mbalimbali kuhusiana na wale wanaoweka Vifaa hivyo jirani na kichwa wakati wa usiku huku wakishauri Watu kuacha utaratibu huo kwani una madhara kiafya.

Sauti za baadhi ya watumiaji wa simu

Taswira ya Habari imezungumza na mmoja wa Wafanyabiashara wa simu na vifaa mbalimbali vya Mawasiliano ambapo amesema sababu kubwa ya Watu wengi kufanya hivyo ni ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya madhara yanayoweza kupatikana.

Sauti ya Mfanyabiashara.