Dodoma FM

Vijana waomba utaratibu mzuri upatikanaji wa fursa

7 August 2023, 5:29 pm

Vijana wanao jihusisha na kazi ya usafirishaji ama bodaboda katika eneo la Majengo sokoni.Picha na Thadei Tesha.

Tarehe 12 Agost ni maadhimisho ya siku ya vijana duniani ambapo pia huadhimishwa kwa kufanya makongamano mbalimbali yenye lengo la kujadili fursa na changamoto zinazowakabili vijana katika maeneo yao.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya vijana jijini Dodoma wameiomba serikali kuweka utaratibu mzuri wa utoaji wa fursa zinazolenga kundi la vijana wahusika waweze kunufaika na uwepo wa fursa hizo.

Dodoma Tv imepita katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dodoma na kushuhudia pilikapilika za maisha za kila siku zikiendelea katika maeneo hayo huku nyingi zikifanywa na vijana.

Kuelekea kuadhimisha siku ya vijana Duniani nawauliza baadhi yao je ni ipi hasa changamoto kubwa inayowakabili ambapo serikali inapaswa kuitazama kwa ukubwa ili wengi waweze kunufaika na kuondokana na hali ngumu ya maisha?

Sauti za vijana.
Picha ni baadhi ya wajasiriamali ambao wengi ni vijana katika soko la Majengo. Picha na Thadei Tesha.

Pamoja na kubainisha changamoto hizo hili  ni ombi lao kubwa  kwa serikali.

Sauti za vijana.

Kata ya Majengo ni miongoni mwa kata ambayo ina mwitikio mkubwa wa vijana wanaofanya biashara na shughuli mbalimbali za kujikwamua kiuchumi hapa namtafuta mwenyekiti wa mtaa huu je ana lipi la kuzungumza kuelekea maadhimisho ya siku ya vijana?

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa.