Dodoma FM

DUWASA yaendelea na ukaguzi miundominu ya maji taka

3 April 2024, 6:13 pm

Picha ni Mafundi kutoka DUWASA wakiendelea na zoezi la ukaguzi wa miundombinu ya maji taka. Picha na DUWASA.

Katika zoezi hilo DUWASA imebaini kuzidiwa na miundombinu ya majitaka eneo la Makole.

Na Seleman Kodima.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imeendelea na zoezi la ukaguzi wa miundombinu ya majitaka katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma ili kuiweka katika hali ya usalama.

Katika zoezi hilo DUWASA imebaini kuzidiwa na miundombinu ya majitaka eneo la Makole kutokana na baadhi ya wananchi kutokuzingatia matumizi sahihi ya miundombinu hiyo kwa kutupa taka ngumu katika chemba za majitaka na hivyo kusababisha kuziba kwa miundombinu ya majitaka.

Meneja wa Majitaka na Usafi wa Mazingira DUWASA, Mhandisi Daniel Mgunda amesema zoezi hilo ni endelevu ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.

Sauti ya Mhandisi Daniel Mgunda.
Picha ni Zoezi la utoaji wa taka ngumu kwenye mifumo ya maji taka likiendelea. Picha na DUWASA.

Naye Rahel Muhando, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma DUWASA, amewataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka kwa usalama wa afya.