Jamii yatakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa
9 June 2026, 18:14

Vile vile ameshauri kutotumia dawa holela bila kupima au kutumia dawa za mtu mwingine ambazo ameacha kuzitumia make zinaweza kuwa zimepoteza ubora na kuzingatia maelezo yaliyowekwa kwenye dawa kufahamu zimetengenezwa lini na muda wa mwisho wa matumizi wa hizo dawa na kutoa taarifa kwa mamlaka pindi mgojwa akiuziwa dawa zilizoisha muda wake.
Na Jerome John.
Jamii Mkoani Dodoma imetakiwa kuzingatia utumiaji sahihi wa dawa wanazopewa na wataalamu wa afya wanapougua na kuanza kutumia dawa hizo.
Akizungumza na Taswira ya Habari Benedict Rashi kutoka mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA,amesema kuwa kutotumia dawa kwa usahihi kunaweza kusababisha usugu wa dawa na kumfanya mgojwa kushindwa kupona au kumfanya mgojwa kubadilishiwa dawa na kuanza kutumia dawa nyingine.
Aidha ametolea msisitizo kuwa sio sahihi kwa mtumiaji wa dawa kupata nusu dozi badala ya dozi kamili na upelekea hizo dawa kushindwa kutibu kabisa ugonjwa na mgonjwa kuanza kulalamika kwanini haponi.
Afisa huyo ametoa rai kwa wauzaji wa dawa kuhakikisha wanafuata miongozo ya tiba wakiwa wanawahudumia wateja wao.