Dodoma FM

Mashamba ya Bangi yateketezwa kwa moto Kiteto

29 April 2026, 16:46

Mashamba hayo yaliyokuwa yamefichwa ndani ya mazao ya mahindi.Picha na Kitana Hamis.

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupambana na matumizi na usambazaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi.

Na Kitana Hamis.
Mashamba makubwa ya bangi yaliyokuwa yakilimwa kwa siri katikati ya mashamba ya mahindi katika Kijiji cha Mbigiri, wilayani Kiteto mkoani Manyara yameteketezwa kwa moto na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa kushirikiana na wananchi.

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupambana na matumizi na usambazaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi, ambayo yamekuwa yakitajwa kusababisha athari kubwa za kiafya na kijamii.

Mashamba hayo yaliyokuwa yamefichwa ndani ya mazao ya mahindi.Picha na Kitana Hamis.

Akizungumza kuhusu operesheni hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Remidius Mwema, amesema namna walivyofanikiwa kubaini mashamba hayo yaliyokuwa yamefichwa ndani ya mazao ya mahindi na kuyateketeza.

Kwa upande wake , Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbigiri, Omari Goda, pamoja na wananchi akiwemo Athumani Dosbori, Asia Salim na Mohamed Zuberi, wamepongeza juhudi za serikali katika kukabiliana na tatizo la madawa ya kulevya, wakisisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia kulinda afya ya jamii na usalama wa vijana.

Sauti ya kina Kitana.