Dodoma FM

Wadau waomba waandishi wa habari kuongeza weledi katika masuala ya jinsia

18 August 2021, 1:04 pm

Na; Mariam Matundu.

Wadau wa masuala ya jinsia wameomba waandishi wa habari Nchini kuongeza weledi katika masuala ya jinsia ili kuondoa mitazamo hasi hasa kwa viongozi wanawake pale wanapofanya nao mahojiano .

Wakizungumza na taswira ya habari wadau hao wamesema baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiuliza maswali ambayo yanaleta ukandamizaji wa kijinsia hasa wanapofanya mahojiano na viongozi wanawake.

Nae chifu mkuu kanda ya kati Dodoma mtemi wa pili mazengo amesema kuwa sera ya hamsini kwa hamsini imeleta mafanikio makubwa katika kupambana na mila potofu zinazomkandamiza mwanamke katika nafasi za uongozi na kwa sasa wanawake wanapewa nafasi.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandaishi wa habari Tanzania TAMWA dkt. Rose Reuben amesema mwanamke anauwezo sawa na mwanaume katika maswala ya uongozi.

TAMWA imewakutanisha waandishi wa habari na wadau wa masula ya jinsia katika kuwajengea uwezo ili kuimarisha weledi wao katika kuripoti habari za kijinsia.