Dodoma FM

CCM Bahi yataka ujenzi wa stendi ya mabasi uchunguzwe

19 April 2023, 12:23 pm

Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Bahi wakiwa katika kikao. Picha na Bernad Magawa.

Suala la changamoto ya stendi mpya ya mabasi wilayani Bahi limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu kutokana na changamoto zilizopo eneo la stendi lakini adha kubwa ikiwa ni ongezeko la nauli mara mbili kutoka Bahi mpaka Dodoma mjini.

Na Bernad Magwa.

Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya Bahi imeiagiza serikali wilayani humo kufanya uchunguzi kuhusiana na ujenzi wa stendi ya mabasi wilayani humo .

Aidha imeagiza kuondoa adha zinazowakabili wananchi ikiwemo ongezeko kubwa la nauli kupitia kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2022 kilichofanyika April 18,2023 wilayani humo.

Akitoa maelekezo hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bahi stuwart Masima amesema kumekuwa na changamoto nyingi kwa wananchi kuhusu stendi hiyo huku akisisitiza kutokuonekana kwa thamani ya fedha iliyotumika.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM wialayani Bahi
Mwenyekiti wa Ccm wilaya ya Bahi stuwart Masima akiendesha kikao Cha halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Bahi. Picha na Bernadi Magawa.

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe.Godwin Gondwe akizungumza baada ya kutolewa maelekezo ameahidi kufanyia kazi maelekezo yote na kuleta taarifa ya utekelezaji wake katika vikao vijavyo.

Sauti ya mkuu wa wialaya ya Bahi

Awali katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Bahi Paulina Lupamba pamoja na wajumbe wengine walipata nafasi ya kutoa michango yao huku wengine wakieleza changamoto zilizopo katika maeneo yao.

Sauti ya katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Bahi