Dodoma FM

Dodoma: Mashine za kuvuna karanga zawakosha wakulima

2 June 2023, 7:06 pm

Mashine ya kuvunia Karanga inayo wawezesha wakulima kuvuna kwa urahisi. Picha na Mindi Joseph.

Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta na zao hili hustawi zaidi katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro.

Na Mindi Joseph.

Wakulima wa zao la karanga mkoani Dodoma wamepongeza uwepo wa teknolijia ya mashine za kuvuna karanga.

Mashine hizi zinawapa wanachi urahisi wa kuvuna tofauti na awali walipokuwa wakitumia jembe la mkono.

Wakizungumza na Taswira ya Habari wakulima hao wamesema hii ni hatua rahisi zaidi katika uvunaji wa zao la karanga.

Sauti za wakulima.
Karanga ambazo tayari zimevunwa na kuanikwa juani ili ziweze kukauka. Picha na Mindi Joseph.

Katibu Mtendaji wa Shirika la DASPA, Aithan Chaula anasema zana hizo zinawapa ahueni wakulima wa zao la karanga kuvana.

Sauti ya Katibu Mtendaji wa Shirika la DASPA.