Dodoma FM

Bodaboda wasabisha kelele walalamikiwa Nzuguni B

15 March 2024, 7:40 pm

Picha ni mwenyekiti mtaa wa Nzunguni B Jackson Chidawali akiongea na Dodoma Tv. Picha na George John.

Pikipiki zimekuwa zikichangia uchafuzi wa mazingira kutokana na kelele.

Na Mindi Joseph.
Wananchi wa Mtaa wa Nzunguni B kata ya Nzunguni Jijini Dodoma wamelalamikia waendesha pikipiki wenye tabia ya kutoboa exsoze za pikipiki na kusababisha vyombo hivyo kutoa sauti zinazo leta kelele.
Ni tabia inayotajwa kushamiri kwa Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda baadhi yao.

Kelele hizo zinaelezwa kuwa na athari kwa jamii na wameomba viongoz kuwapa elimu vijana wa usafirishaji maarufu kama bodaboda pengine wanaweza kubadilisha ama kuacha kabisa tabia hizo.

Sauti wananchi wa Nzuguni B.
Picha ni Mtaa wa Nzuguni B . Picha na George John.

Kwa upande wa mwenyekiti mtaa wa Nzunguni B Jackson Chidawali amesema kero hiyo imekuwepo na wameshachukua hatua ili kukabiliana nayo.

Sauti ya Jackson Chidawali.