Dodoma FM
Dodoma FM
17 April 2026, 5:35 pm

Pamoja na changamoto hizo ndogondogo lakini wananchi baada ya elimu wamekuwa na mwitikio mzuri wa kurasimisha ardhi zao.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa kijiji cha Chinangali ii Kata ya Majeleko wameiomba Serikali kupunguza gharama za urasimishaji ardhi.
Wananchi hao wamesema kuwa ombi hilo linatokana na utofauti wa ukubwa wa maeneo kwani baadhi yao wamekuwa na viwanja vidogo huku bei elekezi ikiwa ni Moja.
Aidha wameiomba mamlaka hiyo ya urasimishaji kuzingatia mipaka ya Kila kiwanja Ili kuondoa migogoro baina ya wananch wenyewe au wananchi na kamati ya urasimishaji.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho bw.Yuda Ndalu ambaye amekiri uwepo wa changamoto za mipaka hususani linapo kuja suala la michoro ya barabara
Amesema kuwa pamoja na changamoto hizo ndogondogo lakini wananchi baada ya elimu wamekuwa na mwitikio mzuri wa kurasimisha ardhi zao.