Dodoma FM

Vitendo vya wizi wa mifugo na ubakaji vimezua hofu mpamaa

14 August 2026, 17:00

Vitendo vya wizi wa mifugo na ubakaji vimewatia hofu na mashaka wananchi wa mpamaa. Picha na mtandao.

Sajent Nichlos ametoa wito  kwa wananchi wa Mpamaa na maeneo jirani kuongeza ulinzi kuwa makini na watu wanaowazunguka na kutoa taarifa mapema pindi wanapoona viashiria vya uhalifu.wananchi nao wanatarajiwa kushirikiana na viongozi pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha vitendo vya wizi wa mifugo vinadhibitiwa na hali ya amani na usalama inarejea katika eneo hilo.

Na Anwary Shabani.

Wizi na ukabaji umeendelea kuibua hofu miongoni mwa wananchi na wafanyabiashara katika eneo la Mpamaa, Kata ya Miyuji, jijini Dodoma, huku baadhi yao wakieleza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwalazimu kuwa na tahadhari kubwa kutokana na vitendo vya wizi vinavyoendelea katika eneo hilo.

Wananchi na wafanyabiashara wa eneo la Mpamaa wanasema hali hiyo imekuwa ikiathiri maisha yao, huku baadhi wakidai kuwa wamekuwa wakiishi kwa hofu ya kuibiwa mifugo pamoja na mali nyingine, jambo linalowafanya wengine kufikiria kuondoka katika eneo hilo.

Aidha  balozi wa mtaa wa Mpamaa Shina namba 4 katika Kata ya Miyuji, Bw. Thomasi Masaka, amesema tatizo hilo limeendelea kwa takribani wiki mbili, akieleza kuwa mifugo kama ng’ombe na mbuzi imekuwa ikiibwa katika eneo hilo.

Pia nae Alen Msese ambaye ni mjumbe wa mpama amesema wizi upon a wimbi hilo limeongeza kutokana na ongezeko la watu katika eneo hilo na kasi ya ukuaji wa jiji la Dodoma ndo sababu moja yapo ya ongezeko la wizi katika eneo la mpamaa.

Kwa upande wa  polisi kata Sajent  Nicholas, Kata ya Miyuji, ambaye kwa hivi sasa amehemishwa kituo kingine ambapo wizi huo umekuwa ukiwaathiri wananchi kwa muda mrefu na  amesema kuwa walikua wakichukua  hatua baada ya kupokea taarifa kuhusu wizi na  katika eneo hilo .

Sauti na Awary Shabani.