Dodoma FM

NGO’s zatakiwa kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za nchi

20 August 2026, 17:03

Wananchi wametakiwa kuendelea kuyaamini mashirika yanayotekeleza shughuli zao kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.Picha na mtandao.

Mashirika yasiyo ya kiserikali ni taasisi zinazofanya kazi kwa lengo la kusaidia jamii na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii katika sekta kama vile elimu, afya, mazingira, kupunguza umaskini na kulinda haki za binadamu.

Na Leokadia Andrew.

Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yamehimizwa kuhakikisha yanafuata taratibu, sheria na kanuni za nchi, huku yakizingatia utamaduni na mila za Watanzania katika utekelezaji wa shughuli zao.

Wito huo umetolewa na BAKARI JUMA, Mwenyekiti wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali Kahama, wakati akizungumza na KM24FM Radio, ambapo amesema baadhi ya mashirika yamekuwa yakipokea fedha kinyume na taratibu zilizowekwa.

JUMA amesema hali hiyo inaweza kuchangia baadhi ya wafadhili kuingiza tamaduni zao katika jamii kupitia miradi na shughuli wanazozifadhili, jambo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa umakini ili kuhakikisha maendeleo yanaenda sambamba na kulinda mila na desturi za Watanzania.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuyaamini mashirika yanayotekeleza shughuli zao kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya mashirika wananchi na mamlaka husika.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameeleza kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa na mchango katika kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali, ikiwemo maendeleo ya kijamii na huduma zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi.

Sauti ya Kulwa.