Wazazi watakiwa kuimarisha malezi ya watoto ili kujenga jamii iliyo bora.
23 September 2026, 16:32

Baadhi ya wadau wa maendeleo ya jamii wamesema wataendelea kushirikiana na wizara hiyo kuhakikisha watoto wanapata malezi bora, huku wakichangia katika ujenzi wa jamii imara na yenye ustawi.
Na Anwary Shabani.
Wazazi wametakiwa kuimarisha usimamizi na malezi ya watoto wao, badala ya kuwaacha bila uangalizi, ili kuwajengea misingi imara na kuwawezesha kukua katika mazingira bora.
Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorth Gwajima, wakati wa mkutano wa nusu mwaka wa tathmini ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, akisisitiza umuhimu wa wazazi kuwa makini katika malezi ya watoto wao.

Aidha, amesema katika kuendeleza mageuzi hayo, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na wadau wake inaandaa ajenda ya mwaka 2050, kwa lengo la kujenga ustawi wa watu na kuimarisha jamii katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.