Dodoma FM

Matumizi ya simu kupita kiasi yanaweza kuathiri maisha ya mtu na jamii

7 October 2026, 16:52

Picha ni mtu anaye tumia simu kupita kiasa, matumizi yasiyo ya lazima kupelekea changamoto ya afya na utendaji kazi. Picha na Tanzania tech.

Matumizi ya simu za mkononi yamekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku, ikiwasaidia wananchi kuwasiliana, kupata taarifa na kujiburudisha, lakini matumizi yake kupita kiasi yameelezwa kuwa yanaweza kuathiri mahusiano ya kifamilia, utekelezaji wa majukumu na ushiriki wa mtu katika jamii.

Na Daniel Njau.

Baadhi ya wananchi wamesema simu zimekuwa na umuhimu katika shughuli zao za kila siku, ikiwemo mawasiliano na burudani, lakini matumizi yasiyokuwa na mipaka yamewafanya baadhi ya watu kutumia muda mwingi kwenye simu kuliko kushughulika na kazi, familia na jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake, Dkt. Andri Godiebo, daktari na mtafiti wa masuala mbalimbali, amesema matumizi ya simu yanapaswa kuwa na mipaka na kutegemea mahitaji ya mtumiaji, ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kiafya na kijamii.

Naye Juma Saidi, anayeeleza kuwa amewahi kutumia simu kupita kiasi bila utaratibu maalumu, amesema matumizi hayo yaliwahi kuathiri mahusiano yake na mzazi wake pamoja na familia yake, hali iliyomfanya kutambua umuhimu wa kuweka mipaka katika matumizi ya simu.

Wataalamu na wadau wa teknolojia wamewataka wananchi,hasa vijana wanaoelekea kujenga familia, kutumia simu kwa malengo yenye tija na kuhakikisha teknolojia haichukui nafasi ya majukumu ya kifamilia, kazi na mahusiano ya kijamii.

Simulizi na Daniel Njau.