Dodoma FM

Matumizi ya skrini muda mrefu yaweza kuhatarisha afya ya macho

8 October 2026, 17:10

Picha ni zoezi la upimaji wa macho likiendelea kwa baadhi ya watu. Picha na Ministry of life.

Wataalamu wa afya wanashauri wananchi kuto kutumia matumizi ya vitu vyenye mwanga mkali kwa muda mrefu kwaajili ya kuepuka magonjwa na kulinda afya ya macho, hivyo wameshauri watu kufanya uchunguzi wa macho kila baada ya muda kutokana na ushauri wa dakatari.

Na Husna Munisi.

Matumizi ya muda mrefu ya simu za mkononi na kompyuta bila kupumzisha macho yameelezwa kuwa yanaweza kusababisha changamoto mbalimbali za afya ya macho, ikiwemo uchovu, ukavu, maumivu na kuona ukungu.

Akizungumzia suala hilo, Daktari wa Macho kutoka CVT Eye Clinic, Dkt. Rajabu Kisonga, amewashauri watumiaji wa vifaa hivyo kuchukua mapumziko mara kwa mara na kuepuka kutazama skrini kwa muda mrefu bila kuyapa macho nafasi ya kupumzika.

Aidha, Dkt. Kisonga amewataka wananchi kutopuuza dalili zinazojitokeza mara kwa mara, zikiwemo maumivu ya macho, kuona ukungu, ukavu wa macho na maumivu ya kichwa yanayoweza kuhusishwa na matumizi ya muda mrefu ya skrini.

Amesisitiza umuhimu wa wananchi kupima afya ya macho mara kwa mara na kufika katika vituo vya afya wanapobaini mabadiliko katika uoni, ili tatizo litambuliwe mapema na hatua stahiki zichukuliwe.

Simulizi na Husna Munisi.