Dodoma FM

Watanzania wanatarajia nini kwenye hotuba ya Rais Samia ?

22 April 2021, 8:39 am

Na; Mariam Kasawa

Rais Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuhutubia Bunge  katika hotuba itakayotoa mwelekeo wa nini hasa amepanga kutimiza katika muhula wake wa kwanza madarakani.

Hii itakuwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo tangu aapishwe kuwa Rais Machi 19 mwaka huu, baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, hayati Dkt. John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu.

Swali kubwa ambalo watu wengi wanajiuliza ni nini hasa Rais Samia atawaambia Watanzania na dunia nzima kwa ujumla leo katika hotuba yake hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa?