Dodoma FM

Mtembezi Marathon kutangaza utalii wa ndani

22 May 2023, 5:53 pm

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri akizungumza katika kikao hicho. Picha na Alfred Bulahya.

Akizungumza baada ya kikao hicho mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh Jabiri Shekimweri amefafanua malengo ya mbio hizo.

Na Alfred Bulahya.

Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Dodoma, Mtembezi Adventures, Pamoja na Dodoma Media Group imeandaa mbio maalum (Mtembezi Marathoni) kwa ajili ya kutangaza utalii wa ndani zitakazofanyika Julai 1 mwaka huu.

Maandalizi ya mbio hizo yameanza kwa vikao mbalimbali ambapo leo kimefanyika kikao maalum kilichojumuisha wadau mbalimbali kujadili namna watakavyoshiriki katika marathoni hiyo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Dodoma.
Mkurugenzi mtendaji wa Mtembezi Adventure akizungumza mara baada ya kikao hicho . Picha na Alfred Bulahya.

Mkurugenzi mtendaji wa Mtembezi Adventure amesema maandalizi ya mbio hizo kwa sasa yamefikia zaidi ya asilimia 50 huku akiwaita wadau na wananchi kwa ujumla kujitokeza kushiriki.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa Mtembezi Adventure .