Dodoma FM

Ujenzi wa madarasa kata ya Suruke wakamilika

10 May 2022, 3:44 pm

Na;Mindi Joseph.

Ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya Msingi Mluwa na sekondari Mto Bubu Kata ya Suruke Wilayani Kondoa yamekamilika baada ya kupata mgao wa shilingi milioni 182 za ujenzi wa madarasa hayo katika kuendelea kuboresha miundombini ya elimu.

Akizungumza na Tswira ya Habari Diwana wa kata ya Suruke Mh Jafari Ganga amesema katika shule ya msingi Tungufu ujenzi wa madarasa matatu unaendelea.

Ameongeza kuwa Mbali na fedha hizo kata hiyo pia imepata shilingi na milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa maabara 2  ambazo zipo hatua ya ukamilishaji.

.

Katika hatua Nyingine amesema wananchi wamekuwa wakiwashirikisha ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa ufanisi.

Aidha amempongeza serikali kwa jitihada inazozifanya katika kuendelea kuboresha miundombinu ya Elimu.