Dodoma FM

Serikali yazindua mfumo wa kielectroniki wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za kiserikali

16 August 2021, 2:12 pm

Na; Fred Cheti.

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri mkuu (Sera ,bunge,kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu) leo Agosti 16 imezindua mfumo wa kielektroniki wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za serikali.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dodoma waziri mwenye dhamana katika wizara hiyo Mh.Jenista Mhagama ambae alikua mgeni rasmi amesema kuwa mfumo huo utaisaidia serikali katika uratibu wa shughuli zote kwa njia ya utendaji na upokeaji wa taarifa sahihi na kwa wakati sahihi katika sekta zote nchini.

Aidha Mh,Mhagama amewataka watendaji wote wa serikali nchini kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao kwa kuwa mfumo huo utakwenda kubaini utekelezaji wa shughuli zote za serikali katika kila sekta hivyo ni lazima kila mmoja ahakikishe anasimamia majukumu yake ipasavyo.

Kwa upande wa wake waziri wa mawasiliano na teknolojia Mh.Faustine Ndugulile ambae alihuhudhuria uzinduzi huo amesema kuwa mfumo huo ni muhimu kwa serikali na kwa wizara yake kwa kuwa unakwenda kutimiza sera ya tehama nchini pia utaongeza uwajibikaji,ufanisi pamoja na uwazi kwa watumishi.

Mfumo huo unatarajia kurahisisha shughuli zote za kiserikali na kuongeza ufanishi kwa watendaji wote katika sekta mbalimbali hapa nchini