Dodoma FM

Mifugo ya mwenyekiti mstaafu yapewa sumu asema anaumuachia Mungu

8 November 2023, 5:21 pm

Katika mkutano huo wananchi hao wameaswa kuwa  kila mwananchi anawajibu wa kuwa mlinzi wa nyumba ya mwenzake.Picha na Full shangwe blog.

Ikumbukwe mtaa huo una mwenyekiti wa mtaa ambapo majukumu yake ni kusimamia na kuhamasisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao na wananchi wana haki na wajibu wa kulinda mali, rasilimali za umma na kupambana na kila aina ya uovu ikiwemo ubadhirifu, wizi ,rushwa na mengineyo kwa mujibu wa sheria

Na Victor Chigwada.

Wito umetolewa kwa wakazi wa mtaa wa Ihumwa A kuwa makini na watu wenye nia mbaya  na wanaojihusisha  na vitendo vya uharifu ambavyo vinahatarisha afya za wanajamii.

Hili linajiri baada ya hivi karibuni kuripotiwa taarifa ya mtu mmoja kusambaza kitu kinachodhaniwa sumu na kusababisha athari kwa mifugo kwa aliyewahi kuwa mwenyekiti wa mtaa huo.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa mtaa huo Bw.Wiliamu Njilimuyi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mtaani hapo na kukemea vitendo hivyo ambapo amesema  kila mwananchi ana wajibu wa kuwa mlinzi wa nyumba ya mwenzake.

Njilimuyi amesema kuwa kwa hivi karibuni watu wasiojulikana wamekuwa wakisambaza vitu vyenye sumu katika nyumba ya mwenyekiti mstaafu Bi.Victoria Joseph ambapo mpaka sasa mifugo kadhaa imekufa kutokana na vitendo hivyo.

Sauti ya Bw.Wiliamu Njilimuyi.

Katika kufahamu undani wa mkasa huo, Taswira ya Habari imezungumza na Bi.Victoria Joseph mwenyekiti mstaafu wa mtaa huo ambapo amekiri  kuandamwa na watu  wanaodhaniwa kusambaza sumu katika nyumba yake huku wakimwaga sumu hiyo kwenye maandazi.

Sauti ya Bi.Victoria Joseph.
wananchi wana haki na wajibu wa Kulinda mali, rasilimali za umma na kupambana na kila aina ya uovu .Picha na Dodoma fm.

Bi.Victoria  amesema vitendo hivyo vimekuwa vikimuumiza  bila kujua nini anaweza kufanya  na ameamua kumuachia Mungu juu ya changamoto hiyo.

Sauti ya Bi.Victoria Joseph.

Kwa upande wao baadhi ya majirani wa Bi.Victoria Joseph wamesema kuwa yaliyomkuta Mwenyekiti huyo Mstaafu yameleta athari kwa majirani wanaomzunguka kutokana na mifugo yao kufa kutokana na sumu iliyosambazwa na watu hao.

Sauti za baadhi ya majirani.