Wananchi watakiwa kuacha matumizi ya dawa bila ushauri wa wataalamu
10 August 2026, 16:24

Wananchi wametakiwa kufuata taratibu sahihi za matibabu, ikiwemo kupata ushauri wa wataalamu kabla ya kutumia dawa na kuzingatia maelekezo waliyopewa.
Na Daniel Njau.
Wananchi wametakiwa kuacha kutumia dawa, hususan antibiotiki, bila ushauri wa daktari na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ili kuepuka madhara na kuongezeka kwa usugu wa dawa mwilini.
Akizungumza kuhusu matumizi mabaya ya dawa,Mtaalamu ya Afya Bwa Abraham Said amesema baadhi ya wananchi hutumia antibiotiki bila kufanyiwa uchunguzi na wengine huacha kutumia dawa kabla ya kumaliza dozi waliyoelekezwa.
Amesema hali hiyo inaweza kuchangia tatizo la usugu wa dawa, jambo linaloweza kufanya matibabu kuwa magumu zaidi.
Baadhi ya wananchi wamesema matumizi ya dawa bila kufuata utaratibu yanachangiwa na sababu mbalimbali, ikiwemo kutotaka kutumia muda mrefu hospitalini na changamoto za kiuchumi. Wamesema wakati mwingine hali ya kipato huwafanya baadhi ya watu kununua dawa kulingana na kiasi cha fedha walichonacho badala ya kufuata maelekezo ya matibabu.