Dodoma FM

Serikali yaanza ukarabati wa miundombinu ya barabara katika kata ya Mtanana

9 August 2021, 1:08 pm

Na; Benard Filbert.

Diwani wa kata ya Mtanana wilaya ya Kongwa Bwana Joel Musa ameishukuru serikali kuridhia kukarabati miundombinu ya barabara hali itakayochagiza maendeleo katika kata hiyo.

Amesema hayo wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu kuanza kutekelezwa kwa ukarabati huo ambapo amebainisha kuwa tayari zabuni zimetangazwa katika gazeti la serikali ili kuwapta wakandarasi watakaosimamia ujenzi huo.

Kadhalika amesema kuwa mwezi wa kumi ukarabati wa barabara utaanza baada ya kukamilika kwa hatua zote.

Amesema kata hiyo inaunganisha barabara kubwa kuelekea wilaya ya kiteto mkoa wa manyara hivyo endapo itakamilika itarahisisha muingiliano wa watu katika shughuli za biashara.

Ukarabati wa barabara katika kata ya Mtanana wilaya ya Kongwa unatarajiwa kuanza mnamo mwezi wa kumi mwaka kwamujibu wa taratibu za kiserikali mwaka wa fedha 2021/2022.