Dodoma FM

Wananchi Ndogowe walalamika kuuziwa mahindi bei ghali

29 March 2023, 2:11 pm

Mahindi yakiwa yamepakiwa kwenye mifuko .Picha na habari leo.

Mfumo huu wa usambazaji wa mahindi ya Bei nafuu unalenga kukabiliana na janga la njaa ambalo pia huchangia kupanda kwa bei ya vyakula.

Na Victor Chigwada.                                                      

Imeelezwa kuwa pamoja na jithada za Serikali kusambaza msaada wa mahindi ya Bei nafuu hususani maeneo ya vijijini lakini baadhi ya watu wametumia Kama fursa ya kuyanunua mahindi hayo kwa bei ya chini na baadae kuyauza kwa bei ya juu

Wananchi wa Kijiji Cha Ndogowe Kata ya Ngh’ambaku Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuhakikisha mahindi hayo ya Bei nafuu yanafika kila kata badala ya kuyasambaza kwa mfumo wa tarafa

Wamesema kuwa msaada huo umekuwa na lengo la kukabiliana na janga la njaa lakini watu wachache wamekuwa wakutumia uwezo wao kuyanunua kwa wingi na baadhi ya wananchi kushindwa kunufaika na msaada huo

Sauti za wananchi.

Bw.Haruni Mlimuka mwenyekiti wa Kijiji hicho anakiri kitendo cha mahindi hayo kufikia sehemu moja imekuwa ikiwakandamiza wananchi wa kata za mbali hali inayo wanufaisha watu wa eneo moja na baadhi ya watu wenye uwezo

Sauti ya Bw.Haruni Mlimuka mwenyekiti wa Kijiji hicho

Mlimuka ameiomba Serikali kusogeza msaada huo kwa kila kata na vijiji Kama ilivyokuwa ikitimia mfumo wa zamani tofauti na mfumo wa kuyafikasha eneo moja la tarafa

Sauti ya Bw.Haruni Mlimuka mwenyekiti wa Kijiji hicho

Aidha pamoja na changamoto hizo lakini imeishukuru Serikali kwa msaada huo wa Hindi ya Bei nafuu na kuwaomba kuongeza nguvu ya kusambaza chakula kutokana na Hali ilivyo kwa Sasa