Dodoma FM

Jamii yaeleza inavyojihusisha kumkomboa mtoto wa kike

11 October 2023, 10:46 am

Picha ni Mkazi wa Jijini Dodoma akiongea na Dodoma Tv juu ya siku ya mtoto wa kike. Picha na Khadija Ayubu.

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa tarehe 19 Desemba 2011 ulipitisha Azimio na kutangaza kwamba, kila tarehe 11 Mwezi Oktoba itakuwa ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike Duniani kote, dhamira ikiwa ni kutambua haki za mtoto wa kike na changamoto za kipekee anazokutana nazo katika maisha.

Na Khadija Ayoub .

Kuelekea wiki ya Maadhimisho ya Mtoto wa Kike Duniani, Baadhi ya wananchi wameelezea jinsi wanavyojihusisha katika kumuwezesha ili kufikia malengo yake.

Hii pia ni fursa kwa wadau wa malezi na makuzi ya watoto wa kike kufanya upembuzi yakinifu kuhusu upatikanaji wa haki msingi za watoto wa kike kwa kukazia: ulinzi, usalama, ustawi na maendeleo na jinsi ya kuboresha haki hizi.

Tarehe 11 Oktoba ya kila mwaka Tanzania uungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambapo lengo la maadhimisho ni kutoa fursa kwa wadau wanaotekeleza afua za watoto hususani watoto wa kike kufanya tathmini ya upatikanaji wa haki, ulinzi na maendeleo ya watoto kwa ujumla na kupendekeza hatua stahiki katika kuboresha huduma hizo.

Hatua hiyo imetusukuma kupitia mtaani na Kuzungumza na baadhi ya wananchi kufahamu wanajihusisha Vipi vipi katika kuwasaidia ili kufikia malengo yao?

Sauti za baadhi ya wananchi.
Picha ni Mkazi wa Jijini Dodoma akiongea na Dodoma Tv juu ya siku ya mtoto wa kike. Picha na Khadija Ayubu.

Aidha Katika kuhakikisha utekelezaji wa afua zinazohusu haki na ustawi na maendeleo ya mtoto zinatekelezwa kwa ufanisi Serikali imeendelea kuboresha huduma za malezi ya watoto wakiwemo wasichana kwa kutoa mafunzo ya malezi chanya kwa wazazi na walezi kwa lengo la kuwezesha makuzi bora ya watoto katika Halmshauri 132 ambapo vikundi vya malezi 1,184 vilianzishwa katika Mikoa 17 ya Tanzania Bara hadi kufikia Juni 2022.

Katika Kufahamu zaidi Mpango wa Serikali katika siku hii ,Dodoma Tv tumezungumza na  Afisa maendeleo jamii mkoa wa Dodoma Bi Hunoratha Rwegasira ambaye ameelezea namna  jamii na serikali inavyosaidia kumuwezesha mtoto wa kike kwenye kufikia malengo yake.

Sauti ya Bi Hunoratha Rwegasira .