Dodoma FM

Idifu waomba kusambaziwa huduma ya umeme

11 April 2024, 5:18 pm

Wananchi wa eneo hilo wanasema huduma ya umeme bado haijafika maeneo mengi. Picha na Facebook.

Tangu REA kusimika nguzo za umeme kwa kufuata muelekeo wa barabara imesababisha baadhi ya maeneo mengi kushindwa kufikiwa na huduma hiyo.

Na Victor Chigwada.
Uongozi wa serikali ya kata ya Idifu wilayani Chamwino umeiomba serikali kuwasambazia huduma ya umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo.

Hayo yamesema na Diwani wa Kata ya Idifu Ndg.Samweli Kaweya wakati akielezea changamoto ya huduma ya umeme ndani ya kata hiyo.

Amesema Tangu REA kusimika nguzo za umeme kwa kufuata muelekeo wa barabara imesababisha baadhi ya maeneo mengi kushindwa kufikiwa na huduma hiyo.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Idifu Ndg.Samweli.
Picha ni Mafundi wakitengeneza nyaya za umeme katika nguzo za umeme . Picha na Facebook.

Kwa upande wao wananchi wametoa kilio chao kwa Serikali na kuihimiza mamlaka husika ya usambazaji kufanya jitihada za kupeleka huduma hiyo.

Sauti za wananchi.