Dodoma FM

Jamii yatakiwa kujenga mazoea ya kutumia maziwa

30 August 2023, 4:58 pm

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wanakiri kutokuwa na desturi ya kunywa maziwa kutokana na sababu mbalimbali . Picha na Aisha Alim.

Daktari Malaki amesema kuwa maziwa hayasaidii kusafisha mfumo wa hewa  kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiamini.

Na Aisha Alim.

Jamii imeshauriwa kujenga mazoea ya kunywa maziwa mara kwa mara ili kuimarisha afya zao kutokana na maziwa hayo kuwa na virutubisho muhimu kwa mwili wa binadamu.

Hayo yameseemwa na Daktari  Malack Malack alipokuwa akizungumza na Dodoma tv na kuwataka wananchi kutumia maziwa kwani yanaimarisha kinga ya mwili na  kuondoa hatari ya uzito mwilini.

Sauti ya Daktari  Malack .
Dkt Malaki Bayaga akizungumza na Dodoma Tv kuhusu faida za maziwa.Picha na Aisha Alim.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na kituo hiki juu ya mwenendo wa utumiaji maziwa licha ya kutambua faida zake kiafya pia wameeleza kutokuwa na desturi ya kunywa mara kwa mara kutokana na sababu.

Sauti za baadhi ya wananchi.

Hata  hivyo daktari Malaki amesema kuwa maziwa hayasaidii kusafisha mfumo wa hewa  kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiamini juu ya dhana hiyo.

Sauti ya daktari Malaki.