Dodoma FM

Kakakuona aonekana katika kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino

7 April 2023, 5:51 pm

Huyu ni mnyama Kakakuona akiwa katika kijiji hicho cha Makang’wa.Picha na Mindi Joseph.

Mnyama huyu wa ajabu ana uwezo wa kujiviringisha kama mpira hasa anapokuwa hatarini, mgongo wake umefunikwa na magamba makubwa na magumu.

Na Mindi Joseph.

Mnyama Kakakuona ambaye ni nadra sana kuonekana hadharani ameonekana katika kijiji cha makang’wa iliyopo katika wilaya ya Chamwino Mkoani  Dodoma ikiwa ni zaidi ya miaka 40 imepita.

Wananchi wa Makang’wa wanasema tangu enzi za mababu anapoonekana mnyama huyo basi mila na desturi zao ni ishara ya kupata ubashiri wa Mvua na Mavuno kwa siku zijazo.

Sauti za Wakazi wa Makang’wa
Wakazi wa kijiji hicho wakiwa wamekusanyika pamoja kwaajili ya kumtazama mnyama huyo.Picha na Mindi Joseph.

Aron Lucas ni mkazi wa Makang’wa ndiye aliyemkamata mnyama huyu anasimulia ilivyokuwa.

Sauti ya Aron

Kuonekana kwa mnyamaKakakuona kunaashiria nini? Chief Tupa wa Makag’wa anaeleza.

Sauti ya Chief Tupa wa Makag’wa

Mnyama huyu wa ajabu ana uwezo wa kujiviringisha kama mpira hasa anapokuwa hatarini, mgongo wake umefunikwa na magamba makubwa na magumu, april 8 chief Tupa atamkabidhi kwa Mamlaka ya Maliasili na Utalii .