Dodoma FM

Timu ya madaktari bingwa kuweka kambi Makole na Mkonze

24 May 2023, 6:56 pm

Picha ni kituo cha afya Mkonze kilichopo kata ya Mkonze Jijini Dodoma. Picha na Fred Cheti.

Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma kutoka kwa madaktari hao.

Na Fred Cheti.

Timu ya madaktari bingwa  kutoka sehemu mbalimbli nchini inatarajia kuweka kambi ya siku mbili katika vituo vya afya vya Makole na Mkonze kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa afya katika vituo hivyo.

Mganga mkuu kutoka jiji la Dodoma Dkt. Andrew Method anaelezea lengo la ujio wa madakatari hao katika vituo hivyo vikubwa vya afya katika jiji la Dodoma.

Sauti ya Mganga mkuu jiji la Dodoma
Mganga mkuu kutoka jiji la Dodoma Dkt. Andrew Method . Picha na Fred Cheti.

Dkt. Methew ametoa wito kwa wananchi jijini  Dodoma kutumia nafasi hiyo kufika katika vituo hivyo ambapo wanaweza kupata huduma kupitia madakatari hao bingwa zikiwemo za mama na mtoto.

Sauti ya Mganga mkuu jiji la Dodoma.