Dodoma FM

Wasimamizi ujenzi wa kituo cha Afya Nkuhungu wapewa wiki tatu kukamilisha

27 April 2023, 6:13 pm

Mkuu wa wialaya ya Dodoma mh. Jabir Shekimweri akizungumza na wakazi wa Nkuhungu. Picha na Mariam Kasawa.

Kituo hicho pindi kitakapokamilika kinatarajia kuhudumia zaidi ya wananchi elfu 40 wa kata ya Nkuhungu.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh Jabir Shekimweri amewataka wasimamizi wa ujenzi wa  mradi wa kituo cha afya Cha Nkuhungu ndani ya wiki tatu wawe wamehakikisha kituo hicho kinaanza kutoa huduma kwa wananchi.

Mh. Shekimweri amesema hayo leo wakati akiweka jiwe la Msingi Katika Kituo hicho ambacho awali kilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kama zahanati kabla ya halmashauri ya jiji la Dodoma kuunga mkono juhudi hizo na kutoa fedha ili mradi huo ujengwe kama kituo cha afya.

Sauti ya Mkuu wa wialaya.
Mh. Mkuu wa wilaya akiweka jiwe la msingi katika kituo hicho cha Afya . Picha na Mariam Kasawa.

Kituo hicho pindi kitakapokamilika kinatarajia kuhudumia zaidi ya wananchi elfu 40 wa kata ya Nkuhungu kama anavyosoma taarifa ya mradi huo Bi Mwasiti Abdala ambae ni Afisa mtendaji wa Kata ya Nkuhungu.

Sauti ya Afisa mtendaji kata.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Nkuhungu Bwn. Mkhandi Daudi Nae alikua na haya kuelezea kuhusu uwepo mradi huo wa kituo cha afya katika kata yake.

Sauti ya Diwani wa kata ya Nkuhungu