Dodoma FM

Taasisi  binafsi zafundwa uandaaji wa mipango kazi

12 December 2023, 8:40 pm

Picha ni baadhi ya washiriki kutoka Taasisi na Asasi mbalimbali walio hudhuria mafunzo hayo. Picha na Mariam Kasawa.

Mafunzo hayo yamewakutanisha wadau kutoka Asasi na Taasisi mbalimbali jijini Dodoma ili kuwajengea uwezo kuhusu upangaji wa mipango itakayo wawezesha kufanya kazi zenye tija kwa jamii.

Na Mariam Kasawa.

Taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali yametakiwa kuandaa mipango kazi itakayo wawezesha kufanyakazi kwa mipango na malengo.

Ni katika mafunzo ya namna ya upangaji wa miradi ya Asasi za kiraia yalio fanyika leo katika ukumbi wa African dream yalio wakutanisha wadau mbalimbambali wa Asasi hizo ili kujengewa uwezo wa namna bora ya kupanga miradi yao.

Akizungumzia lengo la mafunzo hayo Bw. Nicolous Mhozya kutoka shirika la Foundation for civil society Dodoma amesema si Taasisi zote ambazo hufuata mipango na kuifanya kuwa muongozo wao hivyo ni vema wakaelewa umuhimu wa kufuata mipango hiyo ili shughuli za Taasisi zao zilete tija katika jamii.

Sauti ya Bw. Nicolous Mhozya.
Picha ni Bw. Nicolous Mhozya kutoka shirika la Foundation for civil society Dodoma akizungumzia kuhusu mafunzo hayo . Picha na Mariam Kasawa.

Nao baadhi ya washiriki walio hudhuria mafunzo hayo wamekiri kunufaika na elimu ya uandaaji wa mipango huku baadhi yao wakikiri kuwa hapo awali walikuwa hawana utaratibu wa kufuata mipango wanayo panga katika Taasisi zao.

Sauti za baadhi ya washiriki.