Dodoma FM

BMH yatoa mkono wa Eid kwa watoto yatima

11 April 2024, 5:41 pm

Picha ni Mkurugenzi mtendaji wa hospital hiyo ,Dkt Alphonce Chandika akiongea baada ya kukabidhi vitu hivyo.Picha na Mariam Kasawa.

Kituo Rahman kinachopatikana Chang’ombe kilianzishwa mwaka 1998 kwa ajili ya kutatua changamoto za akina mama ambapo mwaka 2006 kilianza kutoa malezi kwa watoto 15 wanaopitia changamoto mbalimbali.

Na Mindi Joseph.
Hospital ya Benjamin Mkapa imetoa vyakula kwa kituo cha Yatima cha Rahman cha Chang’ombe jijini Dodoma kama sehemu ya kusheherekea Sikukuu ya Eid -el-Fitr.

Kituo hicho chenye watoto 150 wamepokea msaada huo wa Vyakula ambavyo vimejumuisha mbuzi wawili ,kilo 50 za mchele, kilo 50 za unga wa ngano, juisi katoni 10 na maji katoni 20 .

Akikabidhi vitu hivyo Mkurugenzi mtendaji wa hospital hiyo ,Dkt Alphonce Chandika amesema pamoja na kutoa huduma za afya ni wajibu wao kurudisha kwa jamii na kulea jamii inayowazunguka.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa hospital hiyo ,Dkt Alphonce Chandika.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Kituo Rukia Hamis ameishukuru hospital ya Benjamin Mkapa kwa msaada huo na kuziomba Taasisi nyingine ziige mfano huo kwa kuwakumbuka watoto yatima nyakati za sikukuu ili watoto hao nao waweze kufurahia kama wengine.

Sauti ya mkurugenzi wa Kituo Rukia Hamis .