Dodoma FM

Wafanyabiashara wa soko la Mavunde waomba kuboreshewa miundombinu

30 May 2023, 5:33 pm

Mwonekano wa soko hilo la Mavunde lililopo Chang”ombe jijini Dodoma. Picha na Thadei Tesha.

Hili ni soko la Mavunde ambalo lipo katika kata ya Chang’ombe jijini Dodoma ambapo miongoni mwa bidhaa zinazopatikana sokoni hapo ni pamoja na mbogamboga na matunda.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Mavunde lililopo Chang’ombe jijini Dodoma wameelezea baadhi ya changamoto zinazowakabili katika soko hilo huku changamoto kubwa ikiwa ni miundombinu ya soko hilo kutokuwa rafiki.

Dodoma Tv imewatembelea baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo na kuzungumza nao ambapo wamesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni pamoja na paa la soko hilo kutokuwa imara jambo ambalo linaweza kuhatarisa usalama wao wakati wa upepo mkali.

Sauti za Wafanyabiashara.
Muonekano wa soko hilo la Mavunde lililopo Chang”ombe Jijini Dodoma. Picha na Thadei Tesha.

Aidha pamoja na suala hilo wameiomba serikali kujenga kituo kwa ajili ya kuchukulia mzigo kwani kwa sasa wanapitia changamoto ya kufuata mizigo umbali mrefu katika masoko ya mjin i ikiwemo soko la sabasaba na hivyo kutopata faida.

Sauti za Wafanyabiashara.