Dodoma FM

Viongozi mbalimbali, wasanii Watoa heshima zao Mwisho

25 March 2021, 1:30 pm

Na; Mariam Kasawa.

viongozi, wasanii na maelfu ya wananchi wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati Dkt. Magufuli kijijini chato mkoani geita

Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na Makamu wapili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdullah wameongoza zoezi la kumuaga Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Magufuli uliopo wilayani Chato Mkoani Geita.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Makamu wapili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar wakitoa heshima zao za mwisho.

Viongozi mbalimbali wakitoa heshima zao za Mwisha kwa mwili wa aliye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Makamanda wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Uwanja wa Magufuli kijijini
 Chato mkoani Geita leo Machi 25, 20121